Shirika la kazi duniani ILO limesema mamilioni ya watu ulimwenguni wamepoteza ajira zao au kupunguziwa muda wao wa kufanya kazi kufuatia janga la virusi vya Corona. 

Katika ripoti yake ya tathmini iliyotolewa leo shirika hilo la kimataifa limeeleza kwamba, ikiwa janga hilo halitoongezeka soko la ajira linapaswa kuanza kurudi kwenye hali nzuri katika kipindi cha nusu ya pili ya mwaka. 

Hata hivyo kwa mujibu wa shirika hilo katika mwaka 2020 asilimia 8.8 ya masaa ya kufanya kazi kwa watu duniani yalipotea. 

Watu milioni 220 duniani kote huenda wakakosa ajira mwaka huu na watu milioni 205 wakakosa ajira mwaka ujao.