Serikali  imeanza  kutekeleza mikakati yenye lengo la  kuweka mazingira mazuri kwa Wakulima kupata mikopo, kwa ajili ya kuendesha shughuli zao.

Kauli hiyo imetolewa jana na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Bungeni jijini Dodoma na kuongeza kuwa, miongoni mwa mikakati hiyo ni kuanzisha dawati la kuwasaidia Wakulima  kuandika  andiko la kuomba  mikopo katika mabenki.

Akijibu maswali ya Papo kwa Papo  kwa Waziri Mkuu, Waziri Mkuu Majaliwa ameziagiza halmashauri  zote nchini kuwa  na dawati  maalum  la  kuwasaidia  wakulima  kuandika  andiko la  kuomba mikopo  benki kwani  kuna  wakulima  wengi  ambao  hawawezi   kufanya hivyo.   

     
Amesema tayari Serikali  imeanzisha benki  maalum ya kilimo ambayo kazi yake kubwa ni kuwasaidia Wakulima.

 Waziri Mkuu Majaliwa alikuwa akijibu swali la Mbunge wa viti maalum  Jackline  Kahinja   aliyetaka  kufahamu Serikali  ina mikakati   gani  kuhakisha  sekta ya kilimo inakua na inamnufaisha mkulima pamja na Taifa.