Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limesema kuwa linamshikilia kijana mmoja aliyefahamika kwa majina ya Shedrak Kapanga (34), amabye alikuwa ni msaidizi wa kazi za ndani kwa tuhuma za kumuua bosi wake na watoto wake wawili  katika maeneo ya Masaki wilaya ya Kinondoni mkoani Dar es salaam.


Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam Muliro Jumanne  amesema kuwa, mtuhumiwa huyo alikamatwa eneo la Magomeni akiwa katika harakati za kutoroka.

Amesema Shadrack Kapanga amekamatwa akiwa na baadhi ya vitu alivyoviiba ndani ya nyumba iliyokuwa ikiishi familia hiyo baada ya kufanya tukio hilo.

Kwa mujibu wa Kamanda Muliro, upelelezi wa tukio hilo unaendelea ili kufahamu sababu za mauaji hayo na pindi utakapokamilika muhusika ama wahusika watafikishwa mahakamani.