Mfanyabiashara Habinder Sethi, ameachiwa huru na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, leo Juni 16, kwa sharti la kulipa Sh. 26.9 bilioni, ndani ya miezi 12, ikiwa ni utekelezaji wa ‘Plea Bargain’ aliyofanya na DPP, Sylveter Mwakitalu, ya kumaliza kesi ya uhujumu uchumi iliyokuwa inamkabili.

Seth ameachiwa baada ya kulipa milioni 200 ambapo pesa zilizobaki atalipa kwa awamu kulingana na makubaliano baina yake na Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) ambapo atatakiwa kulipa kwa kipindi cha miezi 12 (mwaka mmoja).

Uamuzi huo umetolewa  na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Huruma Shaidi wakati kesi hiyo ya Uhujumu uchumi namba 27/2017 ilipoitwa mahakamani hapo kwa makubaliano.