Viongozi wawili kati ya 36 wa Jumuiya za Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI), Sheikh Farid Hadi Ahmed na Mselem Ali Mselem waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya ugaidi wameachiwa huru.

Viongozi hao wameachiwa huru baada ya Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka kuwafutia mashtaka viongozi wote wa jumuiya hiyo na kilichobaki sasa ni taratibu za kutoka gerezani.

Msemaji wa Shura ya Maimamu Tanzania Ibrahim Zuberi Mkondo amesema kuwa, tayari Sheikh Farid na Sheikh Msellem wamesafirishwa kwa ndege kwenda Zanzibar.

Viongozi hao wawili na wenzao walikuwa mahabusu tangu mwaka 2014 kutokana na kukabiliwa na mashtaka hayo ya ugaidi ambayo hayana dhamana.