Mahakama Kuu imetengua hukumu ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliyowatia hatiani Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na wenzake saba, na kumriwa kulipa faini TZS milioni 350 au kwenda jela kwa miezi mitano kila mmoja.

Mbali na kutengua hukumu hiyo, Mahakama Kuu imemauru viongozi hao kurejeshewa faini TZS milioni 350 waliyolipishwa baada ya kutiwa hatiani.


Uamuzi huo umetolewa leo Ijumaa, tarehe 25 Juni 2021 na jaji wa mahakama hiyo, Irvin Mgeta, akisoma hukumu ya Rufaa Na. 76/2020, iliyowasilishwa na Mbowe na wenzake, kupinga hukumu hiyo iliyotolewa tarehe 10 Machi 2020 na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba.

Mbali na Mbowe, warufani wengine katika rufaa hiyo ni, Katibu Chadema, John Mnyika na Naibu Katibu Katibu Mkuu wa chama hicho Zanzibar, Salum Mwalimu.

Wengine ni waliokuwa wabunge wa Chadema, Halima Mdee (Kawe), Ester Bulaya (Bunda), Esther Matiko (Tarime Mjini), John Heche (Tarime Vijijini) na Peter Msigwa (Iringa Mjini).