Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imesema kuanzia kesho Jumatano Juni 23, 2021 itakuwa ni marufuku kwa mtu yeyote kuingia eneo la hospitali hiyo au kutoa huduma bila kuvaa barakoa na mgonjwa atatakiwa kuwa na msindikizaji mmoja tu.

Taarifa iliyotolewa leo Jumanne Juni 22, 2021 na mkuu wa kitengo cha mawasiliano kwa umma wa MNH,  Amaniel Aligaesha inaeleza kuwa hatua hizo zinatokana na maagizo ya waziri wa afya kwa taasisi mbalimbali akizitaka kuchukua tahadhari ili kujikinga na kuwakinga wananchi dhidi ya wimbi la tatu la ugonjwa wa Uviko-19 (Covid-19).