Isaac Herzog mwanasiasa mkongwe na mtu maarufu miongoni mwa waisrael amechaguliwa rais mpya wa Israel nafasi ambayo haina mamlaka makubwa lakini yenye lengo la kutoa dira ya kimaadili na kuimarisha mshikamano. 

Wabunge 120 wa bunge la nchi hiyo wamepiga kura ya siri kuchagua kati ya mwanasiasa huyo na Miriam Peretz ambaye hajulikani katika jukwaa la siasa za nchi hiyo lakini mtu mnyenyekevu. 

Herzog mwenye umri wa miaka 60 aliwahi kuwa kiongozi wa chama cha Labor na kiongozi wa upinzani aliyewahi kushindwa na waziri mkuu Benjamin Netanyahu mwaka 2013 katika uchaguzi wa bunge. 

Rais huyo mteule anatokea kwenye familia maarufu ya mrengo wa vuguvugu la msimamo mkali la kizayuni na babaake Chaim Herzog aliwahi kuwa balozi wa Israel katika Umoja wa Mataifa kabla ya kuchaguliwa rais. 

Isaac Herzog atakuwa rais wa 11 wa Israel akitwaa nafasi ya rais Reuven Rivlin anayeondoka mwezi ujao baada ya miaka saba ya kukaa kwenye nafasi hiyo ya uongozi.