Ulimwengu wa sasa ni wa utandawazi soko la simu limesaidia kwa asilimia 99% kuifanya dunia tuione kwa udogo wa Kijiji makampuni mengi ya simu yamekuwa yakijitahidi kutengeneza smartphone kwa ubora wa hali ya juu na kwa bei rafiki. Mwaka huu tumeona makampuni mengi kama Infinix, TECNO na Samsung ya kileta simu zenye sifa za kufanana ambazo ni Infinix NOTE 10pro, TECNO Camon 17pro na Samsung Galaxy A52.

Kabla sijaingia ndani zaidi kuzitofautisha kwanza nitataja sifa kuu ya kila simu, Infinix NOTE Pro sifa yake kuu ni MediaTek Helio G95processor, TECNO Camon 17pro sifa kuu MP48 za kamera ya mbele na Samsung ni MP64 za kamera ya nyuma.

Sifa Za Ndani.

Processor

Kwa upande wa processor Infinix Note 10 Pro inatambulika kama simu bora sana kwa ajili ya kucheza game kwani simu hii inakuja na processor ya Helio G95. Kwa mujibu wa tovuti ya nanoreview.net, Infinix Note 10 Pro inauwezo zaidi wa game kuliko Galaxy A52ambayo inakuja na processor ya Snapdragon 720G.

Kama unavyoweza kuona kwenye picha hapo juu, Infinix Note 10 Pro inaonyesha kuwa bora hasa kwenye upande wa game, huku kwenye upande wa performance ikiwa na utofauti wa alama mbili tu na processor ya Snapdragon 720G.


Ram

Kwa upande wa RAM ni wazi kuwa simu hizi zinatofautina kulingana na toleo, lakini kwa upande wa Infinix Note 10 Pro unapata toleo lenye GB 8 za RAM huku kwa Galaxy A52 ukiwa unapata matoleo ya GB 4, 6 na 8. Pamoja na TECNO Camon 17 Pro.

Uhifadhi wa Ndani (Rom)

Kwa upande wa uhifadhi wa ndani au ROM, Infinix Note 10 Pro inaongoza kwenye list hii na kabla hujabisha ngoja nikwambie ni sababu kwa nini. Infinix Note 10 Pro inakuja uhifadhi wa GB 128 na 256 sawa kabisa na simu zote kwenye list hii. Lakini utofauti mkubwa unakuja kuwa, Infinix Note 10 Pro ina uwezo wa kuchukua memory card ya Hadi TB 2 tofauti na Galaxy A52 ambayo inaweza kuchukua Memory ya hadi TB 1.

Mbali na hayo sehemu ya kuweka memory card kwenye Infinix Note 10 Pro imejitenga na hivyo una uwezo wa kuweka laini mbili za simu pamoja na Memory card, huku kwa Galaxy A52 ukiwa na uwezo wa kuweka kati ya Laini ya pili au memory card yani ni lazima kuchagua moja.

Sensor

Kwa upande wa Sensor au sensa simu zote zinakuja na sensa ambazo zinafanana ambazo ni Fingerprint, accelerometer, gyro, proximity, na compass. Tofauti kubwa ambayo ipo kwenye Infinix Note 10 Pro ni pamoja na kuwa na sehemu ya Fingerprint pembeni kwenye sehemu ya kuwasha hii itakupa urahisi wa kufikia sehemu hii hata kwa mkono mmoja tofauti na Galaxy A52 ambayo inayo sehemu ya fingerprint kwenye kioo ambayo ni lazima kushika simu kwa mikono miwili.

Battery

Kwa upande wa battery simu ya Infinix Note 10 Pro inaongoza kwenye upande wa battery kutokana na kuwa na battery kubwa ya 5000 mAh ambayo pia inaweza kujaa chaji kwa haraka kutokana na kuwa simu hii inakuja na teknolojia ya Fast charging ya hadi 33 Wh.

Tofauti na Galaxy A52 simu hii inakuja na battery ya 4500 mAh, ambayo inakuja na teknolojia ya fast charging yenye uwezo wa hadi 25 Wh. Camon 17 Pro yenyewe inakuja na Fast charging yenye uwezo wa hadi 25 Wh.

Kamera

Kwa upande wa kamera simu zote kwenye list hii zipo sawa huku Infinix Note 10 Pro ikiwa na kamera kuu ya Megapixel 64 pamoja na kamera nyingine tatu, za MP 8 (ultrawide), MP 2 (depth) na MP 2 (monochrome). Galaxy A52 na Camon 17 Pro zote zinakuja na kamera kuu za MP 64.

Kwa upande wa selfie, Camon 17 pro inakuja na kamera kubwa ya selfie ya Megapixel 48 huku ikiwa na uwezo wa flash kwa mbele.

Kwa upande wa mfumo, simu zote za Infinix Note 10 Pro na Galaxy A52 pamoja na Camon 17 Pro zinakuja na mfumo mpya wa Android 11. Mfumo huu unakupa nafasi ya kutumia simu ya Android kwa urahisi zaidi huku ukiwa na uwezo wa kutumia programu mbalimbali zaidi ya moja.

Sifa Za Nje

Muundo

Tukianza na muundo simu ya Infinix Note 10 Pro ni simu bora kwenye kipengele hichi, hii inatokana na simu hii kuwa na muundo mkubwa kuliko simu nyingine kwenye list hii na bado kuendele kuuzwa kwa bei nafuu. Infinix Note 10 Pro inakuja na urefu (height) inch 6.80, upana (width) inch 3.08, na kina (depth) inch 0.31.

Galaxy A52 yenyewe vipimo vyake ni urefu inch 6.30, upana 2.96 na kina ni 0.33, mbali na hayo Tecno Camon 17 Pro yenyewe inakuja na urefu inch 6.65, upana ni inch 3.03, na kina inch 0.35.

Kioo

Tukija kwenye upande wa kioo, Infinix Note 10 Pro pia inaongoza kwenye kipengele hichi kwa kuwa na kioo kikubwa zaidi, Infinix Note 10 Pro inakuja na kioo cha inch 6.95, tofauti na simu za Galaxy A52 na Camon 17 Pro ambazo zinakuja na vioo vya inch 6.5 kwa Galaxy A52 na inch 6.8 kwa Camon 17 Pro.

Mbali na hayo Infinix Note 10 Pro inaongoza kwa resolution ikiwa na resolution ya hadi pixel 1080 kwa 2460, huku ikiwa imefungana na Camon 17 Pro. Galaxy A52 ni ya mwisho kwenye kipengele hichi huku ikiwa inakuja na resolution ya hadi pixel 1080 kwa 2400.

Upatikanaji

Kwa upande wa upatikanaji Infinix Note 10 Pro inapatikana kwa urahisi kwa sasa kutokana na kuzinduliwa hivi karibuni, pia inapatikana ikiwa na ofa mbalimbali kama vile of ya GB 78 kutoka Tigo pale utakapo nunua simu hii kwenye maduka yaliyo thibitishwa.

Kwa taarifa zaidi za upatikanaji tafadhali piga nambari ya simu 0744606222.