Mahakama  ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mbeya imeahirisha kusoma hukumu ya kesi ya kada wa Chadema, Mdude Nyangali iliyokuwa itolewe leo Jumatatu Juni 14, 2021.

Hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo,  Zawadi Laizer amesema ameiahirisha kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wake na kubainisha kuwa hukumu hiyo itasomwa Juni 28, 2021. Mdude anakabiliwa na shtaka la kusafirisha heroin gramu 23.4 mwaka 2020.

Akizungumza nje ya mahakama mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amewataka wafuasi wa chama hicho kuwa watulivu mpaka tarehe iliyopangwa.