China imelaani vikali hatua ya Rais wa Marekani Joe Biden ya kusaini amri ya kuziwekea marufuku ya uwekezaji kampuni kadhaa za Kichina za sekta ya ulinzi na teknolojia. 

Katika mkutano na waandish habari, msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Wang Wenbin amesema China inaitaka Marekani kuheshimu sheria ya soko na kuifuta marufuku hiyo. 

"Marekani inapaswa kuheshimu sheria, kuheshimu soko, kurekebisha makosa yake, na kuacha kuchukua hatua ambazo zinaharibu mpangilio wa masoko ya kifedha ya kimataifa na haki na maslahi halali ya wawekezaji", amesema Wenbin. 

Biden alisaini agizo hilo jana, na utawala wake unadai kwamba hatua hiyo ni sehemu ya mchakato wa kuweka sawa utaratibu mbaya wa enzi ya Rais wa zamani Donald Trump.