Watu watatu wanahofiwa kufa katika ajali ya basi la Classic eneo la Buyubi Kata ya Didia mkoani Shinyanga, huku wengine 34 wakijeruhiwa baada ya basi hilo kuacha njia na kupinduka majira ya saa 10:00 alfajiri ya Juni 2, 2021, wakati likitokea Kampala Uganda kuelekea Dar es Salaam.
Baadhi ya maeruhi wa ajili hao wamesema kuwa ajali hiyo imetokea baada ya dereva wa basi hilo kushindwa kukata kona katika barabara ya Shinyanga Kahama na kwamba mara baada ya ajali hiyo dereva alikimbia.
Kwa upande wake Kamanda wa Polisi wa wilaya ya Shinyanga John Kafumu, amefika eneo la tukio na kueleza kuwa taarifa zaidi kuhusiana na ajali hiyo zitatolewa na Kamanda wa Polisi mkoa Debora Magiligimba.