Baada ya Rais Mstaafu wa Afrika Kusini, Jacob Zuma kuhukumiwa kwenda jela miezi 15 na Mahakama ya kikatiba, Mahakama hiyo imempa siku 5 Zuma za kujisalimisha yeye mwenyewe kwenye Vyombo vya Dola ili aanze kutumikia hukumu yake.
Zuma amehukumiwa baada ya kukutwa na hatia ya kukaidi agizo la kufika Mahakamani ili kutoa ushahidi kuhusu shutuma za rushwa wakati wa utawala wake.