Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa amehimiza Wasanii nchini kuhakikisha  wanamiliki Bima za Afya ambazo zitawasaidia wanapokua wagonjwa wakati wowote

Mhe. Bashungwa amesema hayo alipomtembelea  Msanii Mkongwe wa Mziki wa Dansi nchini Kikumbi M. Mpango maarufu King Kikii  Nyumbani kwake Jijini Dar es Salaam  Mei 22, 2021.

"Wizara itaendelea kufuatilia kwa ukaribu matibabu yako na kwasababu daktari wako tuna mawasiliano ya karibu tutakuwa tunajua hali yako inavyoendelea kila siku" alisisitiza Mhe. Bashungwa.

Kwa upande wake Msanii King Kikii amemshukuru Waziri Bashungwa kwa kumtembelea na kumfariji pia amemuomba Waziri amfikishie Salam zake kwa Mhe. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kumpongeza kwa kazi  nzuri ya kuliongoza Taifa.

Mzee King Kikii ametumia nafasi hiyo  kuwaasa wanamziki na wasanii  wengine  kuwa na nidhamu katika kazi ili kuendelea kufanya sanaa kwa muda mrefu.