Watu tisa wamefariki na watoto wawili kujeruhiwa vibaya jumapili baada ya gari la umeme linaloshikiliwa na waya angani kuanguka huko Italia. Gari hilo linaunganisha Ziwa Maggiore na mlima wa karibu katika eneo hilo. 

Gari hilo kwa jina Stresa-Mottarone kwa kawaida linabeba watalii na watu wanaoishi katika mji wa Stresa katika ziwa Maggiore na kawaida linafanya safari hiyo mita 1,400 angani kutoka usawa wa bahari. 

Msemaji wa huduma za uokoaji Simone Bobbio amesema gari hilo lilikuwa limewabeba watu 11. Gari hilo limeanguka kutoka kwenye eneo la juu zaidi la mlima ambalo kwa kawaida linapendwa na watalii.