Wanamgambo wa Hamas wa Palestina wamesema leo kwamba wamefyatua zaidi ya maroketi 200 kuelekea nchini Israel, ikiwa ni hatua ya kulipiza kisasi cha mashambulizi kwenye jengo refu katika mji wa Gaza. 

Ndege ya kijeshi ya Israel imelishambulia jengo la ghorofa tisa katika mji wa Gaza na kulisambaratisha. Jengo hilo lilikuwa la makazi ya watu, makampuni za uzalishaji wa vifaa tiba na kliniki ya meno. 

Ndege hizo zilofyatua maroketi ya onyo kutokea kwenye ndege isiyo na rubani kuwatahadharisha watu kuhusu mashambulizi ya mabomu yaliyofuata, mapema Jumatano hii. Hata hivyo hakukua na taarifa ya majeruhi ama vifo.