Ndege za kivita za Israel zimeendelea na mashambulizi yake mapema leo kwenye Ukanda wa Gaza, huku wanamgambo wa Kipalestina wakizidisha urushaji wa makombora yao kuelekea Israel. 
 
Wizara ya afya ya Gaza imesema kufikia asubuhi ya leo, mashambulizi ya Israel yalishauwa watu 23, tisa kati yao watoto wadogo, huku 107 wakijeruhiwa, tangu mashambulizi kuanza jana Jumatatu. 
 
Hata hivyo, Israel inasema iliowauwa ni wanamgambo 15 tu kundi la Hamas na washirika wake, huku kwa upande wake ikiwa na majeruhi sita. 
 
Afisa mmoja wa Kipalestina ameliambia shirika la habari la Reuters kwamba Qatar, Misri na Umoja wa Mataifa zinajaribu kuingilia kati ili kuyakomesha mapigano yanayoendelea sasa, yanayotajwa kuwa mabaya zaidi tangu yale ya mwaka 2019. 
 
Credit:DW