Waandamanaji 7 wanaopinga utawala wa kijeshi wameuwawa kwa kupigwa risasi na vikosi vya usalama nchini Myanmar. 

Tukio hilo lililoripotiwa na vyombo vya habari nchini humo linatokea miezi mitatu baada ya mapinduzi ya kijeshi ambayo yameliingza taifa hilo katika vurugu.

Idadi kubwa ya waaandamaji ilijitokeza katika miji na majiji ya taifa hilo ikiwemo Yangon na Mandalay.

Kiini cha maandamano hayo ni kuondolewa mamlakani kiongozi wa kiria Aung San Suu Kyi, mwenye umri wa miaka 75, ambae yeye na wenzake kadhaa wa chama chake cha NLD wanashikiliwa na jeshi tangu kufanyika mapidunzi.