Urusi imesema itatuma kile ilichokielezea kama ishara "mbaya" kwa Marekani kuelekea mkutano wa kilele wa viongozi wa nchi hizo mbili mwezi ujao, huku naibu waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Ryabkov akitangaza hatua ya nchi hiyo kuongeza ulinzi wa kijeshi katika mpaka wake wa magharibi. 

Matamshi haya yanakuja siku moja baada ya Rais wa Marekani Joe Biden kusema kuwa atamshinikiza Rais Vladimir Putin kuheshimu haki za binadamu watakapokutana mjini Geneva mnamo Juni 16. 

Ryabkov amesema Urusi imejiandaa kumjibu Biden kuhusiana na masuala ya haki atakayouliza. 

Amesema pia kuwa Urusi iko tayari kwa mabadiliko yoyote katika ajenda ya mazungumzo ya mkutano huo wa kilele kinyume na Marekani. Uhusiano kati ya Urusi na Marekani umeshuka hadi kufukia kiwango cha wakati wa baada ya Vita Baridi.