Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya imependekeza, kwamba raia wa kigeni waliochanjwa kikamilifu dhidi ya COVID-19 na wale wanaowasili kutoka mataifa yenye hali nzuri waruhusiwe kuingia katika kanda hiyo bila vikwazo vya ziada. 

Msemaji wa halmashauri hiyo, Adalbert Jahnz amesema kuwa ruhusa hii inaweza kusogezwa kwa chanjo zilizokamilisha mchakato wa matumizi ya dharura ya Shirika la Afya Duniani, WHO. 

Halmashauri hiyo pia imependekeza kupandisha kiwango cha awali cha idadi ya visa vya COVID-19 kinachotumiwa kuamua orodha ya mataifa ambamo wasafiri wanaruhusiwa kusafiri katika kanda ya Umoja wa Ulaya, na kuongeza kwamba hilo litasaidia kupanua orodha hiyo.