Samirah Yusuph.
Bunda.
Katibu tawala wa  Wilaya ya Bunda Halfan Mtetela ametoa wito kwa wakala wa barabara mjini na vijijini TARURA kufanya marekebisho ya mara kwa mara barabara za ndani ya hifadhi ili kurahisisha shughuli ya utalii.

Wito huo umeutoa jana wakati wananchi wa wilaya ya Bunda walipotembelea hifadhi ya Taifa ya Serengeti  upande wa Kilawira na kusisitiza kuwa  kila mtu ahamasike kutembelea vivutio vya utalii ikiwemo mbuga  za  wanyama na hifadhi za taifa.

“Barabara zikiwa hazijatengenezwa vizuri inakuwa changamoto kupitika ni lazima wakala wa barabara vijijini na mjini (TARURA)  kuona  umuhimu wa kizitengeneza  na ikiwezekana kuongeza bajeti ili kusaidia kwenye matengenezo hayo, zitasaidia  kuvutia watalii na kufika eneo husika kwa urahisi na kwa wakati,”amesema Mtekela.

Alisema Watanzania wanapaswa kuwa wazalendo kwa kupenda  vivutio vyao na kuvitangaza ili  kufanya idadi  ya watanzania wanaotembelea hifadhi na mbinga za taifa iongezeke.

"Kila mmoja anapaswa kuwa balozi wa kutangaza vivutio kwenye mtandano kupokea watalii kutoka ndani na nje  kwani kufanya hivyo kutapelekea kuongeza pato la mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.

Kwa upande wake mkurugenzi wa kampuni ya NCT twende kutalii Albart Chenza alisema katika kuhakikisha watanzania wengi wanatembelea hifadhina vivutio hivyo,kampuni yake kwa kushirikiana na uongozi wa Serengeti wameanzisha mpango wa kutembelea taasisi na wananchi ili kuhamasisha wananchi hao wanatembelea hifadhi hizo

“Hifadhi ya Serengeti imeanzisha mpango unaoitwa mlango kwa mlango…na sisi kampuni yetu tunaunga mkono na kuhamasisha wananchi na mpaka sasa mwamko umeanza kuonekana.

 Nae Gilango Nyarunge mfugaji wa kijiji cha Salangwe Bunda ambaye amepata fursa ya kutembelea hifadhi ya Serengeti alisema amejifunza vitu vingi na kuahidi kuhamasisha wenzake kuwa na desturi ya kutembelea hifadhi hizo.

"Watanzania tupo  zaidi ya milioni 60 kwa sasa lakini ukiangalia idadi ya watu wanaoingia kwenye hifadhi zetu  kuangalia utalii ni wachache kuliko  idadi ya watu waliopo nchini hali hii inaonyesha sisi siyo wazalendo ni  vyema tupende  utalii wa kwetu wa ndani .

mwisho