Kanda ya ziwa Victoria (Mikoa ya Kagera, Geita, Shinyanga, Mwanza, Simiyu na Mara): Vipindi vya mvua na ngurumo za radi katika baadhi ya maeneo.

Nyanda za juu kaskazini-mashariki (Mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro,): Vipindi vya mvua katika maeneo machache.

Pwani ya kaskazini (Mikoa ya Tanga, Maeneo ya kaskazini mwa Morogoro, Pwani na Dar es Salaam pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba): Vipindi vya mvua katika maeneo machache.

Magharibi mwa nchi (Mikoa ya Kigoma, Katavi na Tabora): Vipindi vya mvua zitakazoambatana na ngurumo za radi katika maeneo machache.

Kanda ya kati (Mikoa ya Dodoma na Singida): Maeneo haya yanatarajiwa kuwa makavu kwa ujumla.

Nyanda za juu Kusini-magharibi (Mikoa ya Rukwa, Songwe, Mbeya, Njombe na Iringa): Maeneo haya yanatarajiwa kuwa makavu kwa ujumla.

Pwani ya kusini (Mikoa ya Mtwara na Lindi): Maeneo haya yanatarajiwa kuwa makavu kwa ujumla.

Kanda ya kusini (Mkoa wa Ruvuma na Maeneo ya kusini mwa Morogoro): Maeneo haya yanatarajiwa kuwa makavu kwa ujumla.

Imetolewana; MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA