Spika wa Bunge Job Ndugai, leo Jumatatu Mei 24, 2021  amewaapisha wabunge wawili waliochaguliwa hivi karibuni katika majimbo ya Mkoa wa Kigoma.


Wabunge hao ni Dk Florence Samizi wa jimbo la Muhambwe na Kavejuru Felix wa la Buhigwe,  wote wakitokea CCM.

Wabunge hao  wameapishwa baada ya  ushindi waliopata katika uchaguzi mdogo uliofanyika kwa majimbo hayo kuwa wazi kufuatia kifo cha aliyekuwa mbunge wa Muhambwe,  Atashasta Nditiye na Dk Philip Mpango wa Buhigwe aliyeteuliwa kuwa Makamu wa Rais.