Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi, Ummy Mwalimu ametangaza kutolewa kibali cha ajira za walimu 6, 649  wenye sifa na  wametakiwa kuomba kuanzia leo Jumapili Mei 9 hadi Mei 23,  2021 dirisha la maombi litakapofungwa.

Waziri Ummy pia amesema nafasi ya ajira 2, 726 za watumishi wa sekta ya afya zimetoka na wenye sifa wanatakiwa kuanza leo.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dodoma leo,  Ummy amesema maombi yote katika nafasi hizo yatatolewa kwa mfumo.

Amebainisha kuwa hakuna mtumishi atakayepewa ajira kwa maombi ambayo hayatapitia kwenye mfumo isipokuwa kundi la walemavu pekee  watakaoomba kwa mfumo wa kupeleka barua zitakazopitia ofisi ya waziri mkuu kitengo cha walemavu.

Ajira za walimu zilizotangazwa ni kuanza ngazi ya astashahada kwa walimu wa shule za msingi, stashahada na shahada kwa walimu wa sekondari.