Sekretarieti ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika SADC imeitisha mkutano wa dharura wa utatu wa Jumuiya hiyo wenye lengo la kujadili mapendekezo ya Mkutano wa Kamati ya Mawaziri wa Afya kuhusu hali ya ugonjwa wa COVID – 19.

 Katika Mkutano huo uliofanyika kwa njia ya mtandao Tanzania imewakilishwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula aliyeambatana na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Balozi Joseph Edward Sokoine ambapo takwimu zinaonesha kupungua kwa maambukizi na vifo katika Bara hilo.

Taarifa hiyo imefafanua kuwa katika kipindi cha mwezi Januari hadi May 2021 Bara la Afrika limeripotiwa kuwa na visa vipya arobaini na mbili elfu ambapo vifo vipya ni Zaidi ya elfu moja na hivyo kushauri kuwa mikutano ya Jumuiya hiyo katika ngazi mbalimbali iendelee kufanyika kwa mseto wa ana kwa ana au  kwa njia ya mtandao.

Katika tukio jingine  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula amefanya mkutano kwa njia ya mtandao na Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway Mhe. Ine Eriksen ambaye ameeleza kuridhishwa na hatua mbalimbali zinazochukuliwa na Serikali ya awamu ya tano katika kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji pamoja na masuala ya utawala bora na haki za binadamu

 Pia kabla ya mikutano hiyo Balozi Mulamula amekutana na kufanya mazungumzo na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalowahudumia Wakimbizi Duniani UNHCR Bwana Antonio Jose Canhandula ambapo wamezungumzia masuala mbalimbali yanayohusu mustakabali wa wakimbizi hususani wa kutoka nchini Burundi na kukubaliana kuwa pande zote ziendelee kuwahamsisha Wakimbizi hao kurejea nchini mwa kwa hiari kwa kuwa hali ya kisiasa nchini humo imetengemaa