Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kesho Ijumaa Mei 7, 2021 anatarajia kuzungumza na wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam katika mkutano utakaofanyika ukumbi wa Mlimani City na kuhusisha wazee takribani 900.

Hayo yameelezwa leo Alhamisi Mei 6, 2021 na mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Abubakar Kunenge aliyebainisha kuwa kulikuwa na utaratibu maalum wa kuwapata wazee hao na kwamba wengine wanapaswa kufuatilia mkutano huo kupitia vyombo mbalimbali vya habari.

Kunenge amewaambia waandishi wa habari kuwa, mkutano huo utafanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City kuanzia saa 8 mchana.

Kunenge ametoa wito kwa Wazee waliopata mwaliko wa kushiriki mkutano huo kujitokeza kwa wingi, ili wapate kusikiliza kile ambacho Rais Samia Suluhu Hassan amewaitia.