Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko ya Uteuzi wa Wakuu wa mikoa wawili.
John Mongella aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu atakuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha. David Kafulila aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha atakuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu
Rais Samia amesema hayo leo Jumatano, Mei 19, 2021 wakati akihutubia mara baada ya kumaliza kuwaapisha wakuu wa mikoa na wakuu wa taasisi, Ikulu jijini Dar es Salaam.
“Kuna mabadiliko madogo nimefanya, Kafulila nilimteua kuwa RC Arusha na Mongella kuwa RC Simiyu, nimeamua Mongella kwa sababu ulikuwa unaongoza Mkoa mkubwa basi ukawe RC Arusha na Kafulila kwa sababu ndio anaanza alikuwa RAS basi akawe RC Simiyu.
"Wote mlioapa na mlioteuliwa hongereni sana, nasema hongereni kwasababu Tanzania kuna Watu wengi na 15% wangefaa kuteuliwa lakini mmeteuliwa nyinyi, naamini mnapokwenda kufanya kazi zenu mtasimama na Mungu.
"Baada ya shughuli hizi za kuapishana na kupiga picha Wakuu wa Mikoa na Wateuliwa wengine mtarudi hapa na tutakuwa na kikao cha kazi kwahiyo kwasababu nina mambo mengi ya kuongea na nyinyi leo tuishie hapa tutakutana kwenye kikao cha kazi,” amesema Samia.