Nteghenjw Hosseah, OR-TAMISEMI
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Prof. Riziki Shemdoe amesema uhamisho wa watumishi wa Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa utafanyika mara nne kwa mwaka yaani kila robo ya mwaka husika.

Akizungumza na waandishi wa habari Prof. Shemdoe amesema kila tarehe 10 ya mwezi unaofuata baada ya robo mwaka kwisha uhamisho utafanyika na majina yatawekwa kwenye tovuti ya Ofisi ya Rais-TAMISEMI.

“Robo kwanza ya mwaka yaan Julai – Septemba majina ya uhamisho yatakua yanatoka tarehe 10 October , na robo ya Pili Oktoba – Desemba majina ya uhamisho yatatoka Januari 10.”

Aliongeza kuwa: ” katika robo ya tatu ya Januari- Machi majina ya uhamisho yatatoka April 10 na robo ya mwisho ya Aprili-Juni majina ya uhamisho yatatoka Julai 10.”

Aidha Prof.Shemdoe alibainisha kuwa majina ya watumishi wote watakaohamishwa yatawekwa kwenye Tovuti ya Ofisi ya Rais TAMISEMI ambayo ni https://bit.ly/2wuts81.