Ikiwa ni takriban wiki mbili tangu akutwe na hatia katika mauaji ya Mmarekani Mweusi George Floyd, Derek Chauvin ameomba kesi yake kusikilizwa upya.

Mwanasheria wa Chauvin, Eric Nelson, amesema uendeshaji wa kesi dhidi ya Polisi huyo wa zamani haukuwa na haki akidai kulikuwa na makosa ya kisheria. Hukumu yake inatarajiwa kutolewa mwezi Juni

Kifo cha Floyd kilichotokea Mei 25 mwaka 2020 kiliibua maandamano makubwa Marekani na Nchi nyingine ambapo maelfu ya watu waliandamana kutaka vitendo vya ukatili wa Polisi dhidi ya watu weusi kufika mwisho.