Waziri wa Viwanda na Biashara, Prof. Kitila Mkumbo na Waziri wa Uwekezaji, Mhe. Geofrrey Mwambe kwa pamoja wamekutana leo Mei 11, 2021 na kufanya mazungumzo na Waziri wa Uingereza anayeshughulikia masuala ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje, Jumuiya ya Madola na Maendeleo ya Uingereza, Bw. James Duddridge.
Katika kikao hicho Mawaziri hao wamepata fursa ya kujadili masuala mbalimbali ya kudumisha na kukuza mahusiano ya biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Uingereza hususani kwa bidhaa muhimu za Tanzania kuuzwa nchini Uingereza na kuvutia Uwekezaji mkubwa wa Uingereza hapa nchini.
Kikao hicho kimehudhuriwa pia na Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Prof. Godius Kahyarara pamoja na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Mhe. David Concar.
Picha zote na Eliud Rwechungura.