Na Mwandishi wetu, Dar
Aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge ambae kwa sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma amekabidhi Ofisi kwa Katibu Mkuu mpya wa Wizara hiyo Mhe. Balozi Joseph Edward Sokoine.

Makabidhiano ya ofisi yameshuhudiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb).