Watu wapatao 27 wamekufa kutokana na kimbunga kikali kilichoikumba sehemu ya magharibi ya India. 

Watu wengine 100 hawajulikani walipo baada ya kimbunga Tauktae kupiga nchini India, na kuzidisha maafa katika nchi hiyo wakati inakabiliana na janga la maambukizi ya virusi vya corona yanayoongezeka huku idadi ya watu waliokufa kutokana na ugonjwa wa COVID-19 ikiongezeka katika muda wa saa 24. 

Kutokana na kimbunga hicho, maalfu kwa maalfu ya watu sasa hawapati huduma ya nishati katika eneo la pwani ya Gujarati, magharibi ya India. 

Wataalam wa jiolojia wamesema kimbunga Tauktae kinatokana na dhoruba zinazoongezeka katika Bahari ya Arabia zinazosababishwa na mabadiliko ya hali ya hewa ambapo joto linaongezeka kwenye maji katika bahari hiyo. Kimbunga hicho Tauktae kilikuwa na kasi ya kilomita hadi 185 kwa saa.