Na Miza Kona Maelezo Zanzibar
Makamu wa Kwanza wa Rais Mhe.Othman Masoud Othman ameitaka jamii kufuata miongozo ya afya na kuongeza hamasa ya mapambano ili kujikinga ugonjwa wa Corona nchini.

Makamu wa Kwanza ameyasema huko katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Mjini Zanzibar katika hafla Makabiadhiano ya Vifaa vya haraka vya kupimia Virusi vya Corona, amesema  ni jukumu la kila mtu kuongeza kasi ya mapambano dhidi ya ugonjwa huo .

Amesema Serikali  ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania inachukua jitihada kubwa ya kupambana na ugonjwa Corona nchini, vifaa hivyo vitasaidia kuongeza kasi ya kiwango cha  upimaji wa virusi vya ugonjwa huo katika jamii.

Amefahamisha ugonjwa wa Corona umeathiri kwa kiasi kikubwa duniani hivyo ni vyema kushirikiana wafadhili na wadau mbalimbali katika kujenga miundombinu mizuri ya afya ili kuepukana na maambukizi.

Makamu wa Kwanza amewasisita wafanyakazi wa wizara ya afya kuitumia vyema msaada huo kwa kufikia malengo yaliyokusudiwa.

Akizungumzia kuhusu hali ya maambukizi nchini Makamu wa kwanza amesema kuwa ugonjwa upo lakini hali sio mbaya hivyo amewasisitiza wananchi kuwa watulivu na kutosikiliza taarifa potofu zinazotolewa katika mitandao ya kijamii ili kuepuka taharuki.

Nae Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto mhe. NassorAhme Mazrui amesema ugonjwa Corona ni tishio duniani  ni vyema jamii kufuata maelekezo yanayotolewa na wataalamu wa afya ili kujikinga na maambukizi

Amefahamisha kuwa vifaa hivyo vya kupimia virusi vya Corona ni vyenye ubora wa hali ya juu ambavyo hutoa majibu ya papo kwa papo vitasaidia kugundua kwa haraka wale wenye kupata maambukizi ya ugonjwa huo.

 Mapema Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Supplier CEO Sunjay  C. Patadia amesema kampuni yake ina uwezo wa kutengeneza dawa na vitendakazi vyevye ubora kimataifa na vifa vipo tayari kwa ajili ya kutoa huduma kwa jamii bila madhara.  

Vifaa hivyo vya haraka vya  kupimia Virusi vya Corona vyenye thamani ya Tsh. Miliono 250 vimetolewa na Kampuni ya SD BIOSENSOR na SUPLIER CEO kutoka Korea.