Tatizo la ukosefu/upungufu wa nguvu za kiume ni nini ?
Ukosefu ama upungufu wa nguvu za kiume ni ile hali ya mwanaume kutokuwa na uwezo wa kufanya tendo la ndoa kwa ukamilifu
MAMBO YANAYO SABABISHA UKOSEFU/UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME.
Yafuatayo ni mambo yanayo sababisha ukosefu wa nguvu za kiume
1. MAGONJWA YANAYO SHAMBULIA MFUMO WA DAMU PAMOJA NA MISHIPA YA DAMU.
Damu ndio nishati inayo wezesha maumbile na kuyafanya kuwa imara.
Hivyo basi ili uweze kuwa imara na wenye nguvu, pamoja na kuwa na uwezo wa kumudu na kustahimili tendo la ndoa wakati wowote , basi ni lazima mwanaume awe na mfumo imara wa damu utakao ruhusu kutiririka kwa damu kwenda katika sehemu mbalimbali za mwili
Ili mfumo uweze kuwa imara ni lazima mhusika awe na damu ya kutosha, na pili awe na mishipa ya damu yenye afya.
Katika mwili wa mwanadamu,kuna mishipa inayo tumika kusafirisha damu kutoka katika sehemu moja ya mwili kwenda katika sehemu nyingine ya mwili ikiwemo maumbile ya kiume. Mishipa hiyo ni kama vile vena (veins), atery ( ateri) na capillary ( kapilari )
Mishipa hii ya damu inapaswa kuwa imara na yenye afya njema wakati wote. Mishipa hii ikipatwa na hitilifu, basi itazuia kusafirishwa kwa damu katika sehemu mbalimbali za mwili wa mwanadamu na hatimaye kufanya suala la kuwa na nguvu za kiume kwa mhusika kuwa ugumu kwa sababu ya kushindwa kupeleka damu kwenye mishipa ya kiume.
Magonjwa kwenye mishipa ya damu huzuia kutirika kwa damu kwenye ogani muhimu kama vile moyo, ubongo na figo.
VIASHIRIA VYA MAGONJWA KWENYE MISHIPA YA DAMU.
Utajuaje kwamba una magonjwa kwenye mishipa yako ya damu ?
Ukiwa una matatizo yafuatayo ya kiafya, ni ishara kwamba, una magonjwa kwenye mishipa yako ya damu:
1. Kolestrol ( Ama lehemu kwenye damu )
Kolestrol nyingi kwenye damu, huzuia kutiririka kwa damu. Kolestrol ikizidi kwenye damu, hupelekea kuziba mishipa ya ateri ambayo kazi yake ni kupeleka damu kwenye uume. Matokeo yake ni mhusika kutokuwa na uwezo kwa sababu maumbile ya kiume hayawezi kusimama bila damu kuingia ndani ya mishipa . Hivyo basi pamoja na dawa ya nguvu za kiume, yakupasa kutibu kolestrol. Unaweza kuondoa kolestrol kwenye damu kwa kutumia dawa mbali za asili kama vile mdalasini,uwatu, habbat sodah etc.
2. Shinikizo Kubwa la Damu
Shinikizo Kuu la Damu husababisha mishipa ya ateri ambayo hutiririsha damu iingiayo kwenye uume kuziba na kushindwa kutanuka kwa kiwango inachotakiwa kutanuka.
Pia huifanya mishipa laini katika maumbile ya kiume kushindwa ku-relax na hivyo kushindwa kuizuia mishipa ya vena ya kunyonya damu
Matokeo yake kunakuwa hakuna kiasi cha kutosha cha damu iingiayo kwenye maumbile ya kiume
Pamoja na kutumia dawa ya nguvu za kiume, unapaswa pia kutumia dawa asilia kujitibu tatizo la shinikizo kuu la damu.
3. Ugonjwa wa kisukari :
Ugonjwa wa kisukari ni miongoni mwa vyanzo vikuu vya tatizo la ukosefu wa nguvu za kiume. Kisukari huathiri mishipa ya damu pamoja na usambazaji wa damu kwenye ogani muhimu mwilini kama vile moyo, ubongo, figo na uume.
Kiukweli, mwanaume mwenye kisukari yupo katika risk kubwa ya kupatwa na tatizo la ukosefu wa nguvu za kiume,m tena katika kiwango kikubwa sana.
Unashauriwa pamoja na kutumia dawa ya nguvu za kiume, tumia pamoja na dawa mbalimbali za asili kwa ajili ya kubalance sukari yako mwilini.
5. Ugonjwa wa moyo
Moyo ndio supplier mkubwa wa damu katika sehemu mbalimbali za mwili. Ugonjwa wa moyo hupunguza uwezo wa moyo kusambaza damu kwenye mishipa mbalimbali ya damu na hivyo kuathiri utendaji kazi wa mishipa ya damu kama vile ateri na vena. Matokeo yake ni mishipa hiyo kushindwa kupeleka damu ya kutosha katika maumbile ya kiume pamoja na kushindwa kuifanya mishipa ya kurelax na matokeo yake,. Ukosefu wa nguvu za kiume.