Mkutano wa kilele unaopangwa kati ya Rais wa Urusi Vladmir Putin na Rais wa Marekani Joe Biden huenda ukafanyika kwa njia ya video, kwa kuzingatia mapendekezo ya watalaamu wa magonjwa ya milipuko.

Putin ambaye uko mjini Moscow, amekutana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kwa mkutano wa kilele wa video, ambapo wamewahimiza Waisrael na Wapalestina kusitisha mapigano. 

Msemaji wa Ikulu ya Urusi Dimtry Peskov amesema uamuzi wa kukutana kwa njia ya mtandao ulitokana na janga la corona na mapendekezo ya watalaamu. 

Biden amependekeza kukutana na Putin katika nchi ya tatu, ikiwezekana Ulaya katika msimu huu wa kiangazi, wakati mvutano kati ya Urusi na Marekani ukishika kasi. Urusi mpaka sasa haijaitikia mwaliko. 

Biden anatarajiwa kuzuru Ulaya mwezi Juni kushiriki mkutano wa kilele wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO.