Wabunge wa Somalia wamepiga kura kwa kauli moja kufuta nyongeza ya miaka miwili kwenye muhula wa rais Mohamed Abdullahi Mohamed waliyoidhinisha mwezi uliopita baada ya kuzuka mvutano mkubwa kuhusu suala hilo.

 Zoezi la kura hiyo lilirushwa moja kwa moja na televisheni nchini humo na lilifanyika muda mfupi baada ya rais Mohammed kulihutubia bunge na kutangaza nia ya kuitisha uchaguziwa bunge uliocheleweshwa. 

Mgogoro wa kisiasa umeibua wasiwasi kuwa Waasi wa Al Shabaab wanaweza kutumia nafasi hiyo kuhatarisha hali ya usalama ikiwa Vikosi vya Serikali vitagawanyika.

Watu 60,000 hadi 100,000 walilazimika kukimbia makazi yao kufuatia mapigano ambayo yalichochea hofu ya vita kati ya vikundi vinavyomuunga mkono Rais na vinavyompinga.