Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) limetangaza kuwa sikukuu ya Eid- El Fitr itakuwa tarehe 13 au 14 mwezi huu kutegemeana na kuandama kwa mwezi.

Sherehe za Eid El-Fitr kitaifa kwa mwaka huu zitafanyika mkoani Dar es salaam, ambapo Swala itaswaliwa katika viwanja vya Mnazi Mmoja kuanzia saa 1:30 asubuhi.