Idara  ya Uhamiaji imewasimamisha kazi Askari wake watatu kwa tuhuma za kutumia nguvu kinyume cha sheria na maadili ya kazi zao dhidi ya Mtuhumiwa wa utapeli Alex Raphael Kyai kama ilivyoonekana katika video fupi iliyosambaa.

Mtuhumiwa huyo anadaiwa kulaghai na kupokea fedha kutoka kwa Wateja mbalimbali ili waweze kupata pasipoti kwa haraka pia amekuwa akijitambulisha kama Mtumishi wa Taasisi nyeti ikiwemo TAKUKURU.