Watu wapatao 44 wamefariki kufuatia mkanyagano uliotokea katika sherehe ya kidini iliyohudhuriwa na makumi kwa maelfu ya waumini wa kiyahudi wa madhehebu ya Othodox huko kaskazini mwa Israel. 

Katika tukio hilo lilotokea mapema leo ijumaa,watu wengine kiasi 150 walijeruhiwa.Limetajwa kuwa moja ya tukio kubwa la ajali iliyosababisha umwagikaji damu nchini Israel. 

Kwa mujibu wa mashahidi,mkanyagano huo ulitokea baada ya idadi kubwa ya watu kujaribu kutoka kwenye eneo la tamasha kupitia njia nyembamba. 

Mkanyagano huo umetokea wakati wa sherehe ya kidini inayofanyika takriban siku 30 baada ya pasaka inayoitwa Lag BaOmer iliyowakusanya maelfu ya watu katika eneo la mlima Meron. 

Na mkusanyiko huo ulikuwa wa kwanza wa watu wengi nchini Israel tangu ilipoondowa vizuizi vya kukabiliana na janga la virusi vya Corona.