Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck  Nchemba (Mb) (kushoto), akipokea nyaraka mbalimbali kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bw. Doto James, alipowasili katika Ofisi za Wizara hiyo zilizopo Mtumba, baada ya kuapishwa na Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Ikulu, Chamwino, jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni (Mb), (kushoto) akipokea nyaraka mbalimbali kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bw. Doto James, wakati wa kikao cha menejimenti ya wizara kilichofanyika Mtumba, baada ya kuapishwa na Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Ikulu, Chamwino, jijini Dodoma.

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (kushoto), akizungumza jambo na Katibu Mkuu, Bw. Doto James, baada ya kupokea nyaraka mbalimbali, wakati wa kikao cha menejimenti ya wizara kilichofanyika Mtumba, baada ya kuapishwa na Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Ikulu, Chamwino, jijini Dodoma.

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (kushoto), akizungumza  na viongozi wa Wizara hiyo (hawapo pichani), wakati wa kikao cha menejimenti  katika Ofisi za Wizara hiyo Mtumba jijini Dodoma ambapo aliwahimiza  kufanya kazi kwa ushirikiano kwa maslahi ya Taifa.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni (Mb) akizungumza jambo na viongozi wa Wizara hiyo wakati wa kikao cha menejimenti  katika Ofisi za Wizara  Mtumba, baada ya kuapishwa na Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Ikulu, Chamwino, jijini Dodoma.

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu  Lameck Nchemba (Mb), akiwa katika kikao cha menejimenti ya wizara katika Ofisi za Wizara hiyo Mtumba jijini Dodoma, baada ya kuapishwa na Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Ikulu, Chamwino, jijini Dodoma.

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akipokea shada la maua alipowasili  katika Ofisi za Wizara  zilizopo Mji wa Kiserikali wa Magufuli -Mtumba, baada ya kuapishwa na Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Ikulu Chamwino, jijini Dodoma. Wa pili kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. Doto James.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni (Mb), akipokea shada la maua kutoka kwa mtumishi Bi. Emiliana Shayo, alipowasili  katika Ofisi za Wizara  zilizopo Mji wa Kiserikali wa Magufuli -Mtumba, baada ya kuapishwa na Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Ikulu Chamwino, jijini Dodoma.

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (kulia), akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bi. Mary Maganga na viongozi wengine wa Wizara. Wa pili kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Bi Amina Shaabani, Kamishna wa Fedha za Nje, Bi. Sauda Msemo (wa pili kushoto), alipowasili katika Ofisi za Wizara hiyo zilizopo Mtumba, baada ya kuapishwa na Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Ikulu, Chamwino jijini Dodoma.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WFM-DODOMA)