Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima,Leo amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Marekeni nchini Tanzania Mhe. Donold Wright Kwenye ofisi za Wizara jijini Dodoma.

Katika mazungumzo yao wameongelea vipaumbele vitatu ikiwemo kuboresha afya ya watanzania, Uwekezaji wa kibiashara pamoja na kuwawezesha vijana wa Tanzania kiuchumi.

Katika kikao hicho kilihudhuriwa na Manaibu Waziri Dkt.Godwin Mollel, Mhe. Mwanaidi Khamis pamoja na Katibu Mkuu-Afya Prof. Abel Makubi na Kamishana wa Ustawi wa Jamii Dkt. Naftali Ng’ondi