Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Said Jafo amesema atahakikisha changamoto za Muungano zilisosalia zinapatiwa ufumbuzi.

Ameyasema hayo jana  mara baada ya kuwasili katika Ofisi ya Makamu wa Rais na kukutana na Menejimenti ya Ofisi yake na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira nchini.

“Nashukuru kwa mapokezi mazuri, ila tuchape kazi tunahitaji kupata matokeo chanya kwa kazi tunazo simamia yaani Muungano na Mazingira” Jafo alisisitiza.

Kwa upande mwingine Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Hamad Chande amesisitiza ushirikiano baina ya watumishi katika kuhakikisha malengo ya kudumisha Muungano na kusimamia Mazingira yanatekelezeka.

Akiwasilisha taarifa ya Ofisi yake Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Joseph Malongo amewahakikishia ushirikiano Mawaziri na kuwakaribisha kwa niaba ya watumishi wenzake.