Na.WAMJW-Arumeru
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.Dorothy Gwajima Jana ametembelea Zahanati ya Momela iliyopo kata ya Ngarinanyuki Wilayani Arumeru na kuzunguza na wanakijiji wa kata hiyo pamoja na muwekezaji (Afrika Amini Alama) ambaye amejenga na kutoa Huduma za afya Katika Zahanati hiyo.

Dkt.Gwajima amefika Kwenye Zahanati hiyo baada ya kupata malalamiko toka kwa wakazi hao kwamba muwekezaji huyo amesimamisha baadhi za Huduma za afya na hivyo kuzorotesha Huduma hizo Mara baada ya kutokea mgogoro baina yake na halmashauri hiyo.

Katika ziara hiyo Dkt.Gwajima alipa fursa ya kutoa elimu kwa wananchi juu ya mwongozo wa Ubia na ushirikiano baina ya Sekta ya Umma na sekta binafsi(PPP) Katika kutoa Huduma za afya na ustawi wa Jamii Tanzania