Na Raymond Mushumbusi, WAMJW Dodoma
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto  Dkt. Dorothy Gwajima amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuongeza nguvu katika Wizara hiyo kwa kuzingatia umuhimu wa Sekta ya maendeleo ya jamii.


Dkt. Gwajima ameyasema hayo jijini Dodoma wakati akizungumza na watumishi wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wakati akimkaribisha Naibu Waziri anayeshughulikia Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Mwanaidi Ali Khamis.


Dkt. Gwajima amesema kuwa Maendeleo ya Jamii ni  kitovu cha maendeleo ya taifa na kama Sekta za maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii zikisimamiwa vizuri, sekta zingine nitapata ufanisi na hivyo kuharakisha Maendeleo kwa Taifa zima.


“Sekta ya maendeleo ya jamii ni mbeleko ya maendeleo ya taifa ni muhimu sana katika kuchgangia sekta nyingine kuendelea na kukua katika kusaidia maendeleo ya taifa kwa ujumla” alisema Dkt. Gwajima


Ameongeza kuwa masuala ya maendeleo ya jamii yakikaa sawa matatizo mengi yanayowakumba wananchi kama vile magonjwa hayatapata nafasi.


Dkt. Gwajima amesema kuwa Jamii ikielimika ikielemika itatatua changmoto  zinazoikabili kutoka na elimu aliyoipata kutoka kwa wataalam wa Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii.


“Katika hili sekta ya maendeleo ya jamii ikitumika ipasavyo watu wakaelimika na kujua vitu vingi wataondokana na changamoto nyingi amabazo zinatatulika kwa jamii kupata elimu ya kukabiliana na changamoto hizo kabla hazijaleta madhara katika jamii” alisema Dkt. Gwajima


Kwa upande wake Katibu Mkuu Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamaii Dkt. John Jingu amemuhakikishia Naibu Waziri huyo kufanya kazi kwa kushirikiana ili kuhakikisha matokea na matarajio ya Rais Samia Suluhu Hassan yanafikiwa.


Amesema Maendeleo ya nchi yanahitaji ubunifu na matumizi ya teknolojia na mabadiliko ili kuhakikisha wananchi hawanabaki nyuma.


Ameongeza kuwa hatua ya Mhe.Rais kumteua Naibu Waziri anayeshughukia maendeleo ya Jamii ni ya kujivunia sana na jambo linalofuata ni kuhakikisha maono ya Rais yanatafsriwa kwa kwa vitendo.


“Niseme hii ni fursa ya kutatua changamoto za Watanzania kwa viwango vinavyokubalika lakini zaidi kutimiza matarajio ya Watanzania, alisema Dkt. Jingu.


Akizungumza mara baada ya kukaribishwa Wizarani Naibu Waziri huyo anayeshughulikia Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Mwanaidi Ali Khamis amesema kuwa atafanya kazi kwa ustadi na kwa kasi ili kuhakikisha kuwa sekta anazosimamia zinakuwa na maendeleo na kutoa matokeo chanja na yanayonufaishi jamii.


“Mimi nipo tayari muda wowote na wakati wowote kuwasikliiza na kujifunza pia msiogope tuelekazane kwa lengo la kupeleka mbele kazi za Wizara na kuwahudumia wananchi” alisema Naibu Waziri Mwanaidi


Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto anayeshughulikia Maendeleo ya Jamii Mhe. Mwanaidi Ali Khamis aliteuliwa na Rais wa Jamnhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Samia Suliuhu Hassan Marchi 31, 2021 na kuapishwa April 1, 2021 kushika nafasi hiyo na kabla ya hapo alikuwa Naibu Waziri wa Fedha.