Rais wa Marekani Joe Biden amesema raia wa nchi hiyo waliochomwa chanjo kikamilifu hawahitaji tena kuvaa barakoa wanapokuwa nje. 

Biden ameyasema haya wakati alipokuwa akilihutubia taifa akisema kwamba hatua kubwa zimepigwa katika suala la utoaji chanjo na kwamba hatua kali za uvaaji barakoa zinastahili kulegezwa kwa sasa. 

"Ni wazi sasa kwamba kama umeshachomwa chanjo unaweza kufanya mambo mengi nje na ndani. kwa hiyo kwa wale ambao hawajachomwa chanjo, hasa kama bado ni kijana au unafikiri hauhitaji chanjo, hii ni sababu kuu ya wewe kwenda kuchanjwa sasa hivi."

Kituo cha kudhibiti magonjwa nchini Marekani CDC lakini kimesema ni muhimu kuvaa barakoa bado hasa wanapokuwa katika matamasha na wanapohudhuria michezo. 

Zaidi ya nusu ya Wamarekani kwa sasa wameshachomwa chanjo dhidi ya virusi vya corona. Idadi ya wale wanaokwenda kuchanjwa imeanza kurudi chini ingawa maambukizi pia yanapungua nchini humo.