Syria na Israel zimeshambuliana tena kwa makombora, huku kila upande ukidai kudunguwa la mwenzake mapema alfajiri ya leo. 

Jeshi la Israel  limesema kombora lililorushwa kutoka Syria limepiga karibu na kinu cha nyuklia katika mji wa Negev ulio kusini mwa Israel.

Kwa mujibu wa jeshi hilo, nalo lilijibu kwa kuishambulia mitambo ya ulinzi na iliyorusha kombora hilo nchini Syria.Kwa upande wake, vyombo vya habari vya Syria vimeripoti kwamba jeshi la anga limeyadunguwa makombora ya Israel yaliyokuwa yameelekezwa kwenye viunga vya mji mkuu, Damascus. 

Kwa mujibu wa wizara ya ulinzi ya Syria, wanajeshi wake wanne wamejeruhiwa na kuna madhara madogo kwenye eneo makombora hayo yalipoangukia. 

Inashukiwa kuwa mashambulizi yaliyoelekezwa nchini Israel yamefanywa na vikosi vitiifu kwa Iran nchini Syria, kulipiza kisasi mashambulizi ya Israel wiki iliyopita dhidi ya kinu cha nyuklia nchini Iran.