Msanii Zuwena Mohamed 'Shilole' amethibitisha kufunga ndoa ya siri na mume wake Rajab Issa maarufu kama Rommy kama ambavyo ilikuwa inaelezwa na baadhi ya vyombo mbalimbali.

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram muda mfupi uliopita Shilole ameandika hilo baada ya kufunga ndoa na mume wake.

"Alhamdulillah tumemaliza salama, rasmi ni mume na mke niliechukuliwa kwa furaha na upendo wa juu 'Officially Husband and Wife happily taken and very much in love' kwasasa unaweza kuniita Mrs Rajab Issa (Rommy) Yarabbi iwe salama".

Kabla ya hapo Shilole alikuwa kwenye ndoa na mfanyabiashara Uchebe na waliachana mwaka jana baada ya ugomvi mkubwa uliotokea kwenye ndoa.