Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA), imesitisha kwa muda matumizi ya bei mpya ya vifurushi vya data ili kutoa nafasi kwa watoa huduma kupanga upya bei za vifurushi kwa ufanisi na kufanya uchambuzi wa kina kwa ajili ya kulinda maslahi ya watumiaji.

Hatua hiyo imechukuliwa ikiwa  ni muda mfupi baada ya kampuni za mawasiliano ya simu kutoa maboresho ya vifurushi ambavyo vimeanza kutumika  Aprili 2, 2021, ikiwa ni sehemu ya matakwa ya kanuni ndogo za vifurushi.

Baada ya vifurushi vipya kutolewa, baadhi ya wananchi kupitia mitandao ya kijamii wamelalamikia kile walichoeleza kuwa ni kupanda kwa gharama za vifurushi, tofauti na matarajio yao kuwa gharama zingepungua.