Rais Samia Suluhu Hassan amesema kuwa anakusudia kuunda kamati ya Wataalamu ambayo itamshauri juu ya hatua za kuchukua dhidi ya ugonjwa wa COVID19.

Rais amebainisha hilo mara baada ya kuwaapisha Viongozi mbalimbali Ikulu jijini Dar es salaam.

"Suala la Covid 19 nafikikiria niunde Kamati ya Wataalamu waliangalie kwa upana wake kitaalamu halafu watushauri Serikali, halifai kulinyamazia aidha kulikataa au kulikubali bila kufanya Tafiti za kitaalamu.

“Tutaunda Kamati ya Wataalamu kuhusu Covid 19 watuambie kitaalamu hayo yanayopendekezwa na Ulimwengu kuja kwetu yapoje, hatuwezi kujitenga tu kama Kisiwa na hatuwezi kupokea yanayoletwa bila kuweka cha kwetu, bila kufanya utafiti wa kwetu.

“Rais Mstaafu  Kikwete alituambia akili za kuambiwa changanya na zako, tuweke na zetu tuwe na msimamo maalum unaoeleweka, sio tunasoma tu mambo ya Covid 19 Ulimwenguni, Tanzania deshi deshi deshi haieleweki, tueleweke kama tunakubali au tunakataa” Amesema Rais Samia