Rais wa Marekani, Joe Biden amesema mkosoaji wa serikali ya Urusi Alexei Navalny, ambaye madaktari wake wameonya kuwa yuko hatarini kupata mshituko wa moyo kutokana na kugoma kula, kwamba hali yake "isiyofaa kabisa."

Alipoulizwa na waandishi habari kuhusu hali ya Navalny ambayo inaripotiwa kuwa mbaya akiwa kizuizini, Biden alisema kuwa "ni mbaya na haifai kabisa." Madaktari wake wamewataka maafisa wa gereza kuwapa ruhusa ili kumfikia haraka iwezekanavyo.

Navalny, mwenye umri wa miaka 44 alifungwa gerezani mnamo mwezi Februari na anatumikia kifungo cha miaka miwili na nusu jela kwa mashtaka ya zamani ya ubadhirifu.

Mnamo Machi 31, mkosoaji huyo wa Rais Vladimir Putin aliamua kugoma kula ili kuishinikiza serikali kumpa matibabu sahihi ya maumivu ya mgongo na ganzi kwenye miguu na mikono.